ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora yaanza Shamrashamra za Miaka Ishirini tangu kwa kupanda miti.

21 Sep, 2022
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora yaanza Shamrashamra  za Miaka Ishirini  tangu kwa kupanda miti.

Serikali  imeipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kuhamasisha jamii kupanda na kutunza ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka ishirini tangu  kwa  kuanzishwa  kwa Tume hiyo.

Hayo alisema  Naibu  Katibu Mkuu,Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu kazungu wakati wa shughuli ya kupanda miti iliyofanyika Septemba 10,2022 katika  Viwanja vya Kwa Swai Jijini Dodoma.

Dkt Kazungu alisema kuwa hatua iliyochukuliwa na Tume itasaidia kukuza uelewa wa jamii juu ya wajibu wao wakupanda  na kutunza  miti kwa manufaa yao na Taifa kwa Ujumla.

“Napenda kutumia nafasi hii kuipongeza Tume,kwani jambo  hili ni utekelezaji wa maagizo ya ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassani kuhusu umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na misitu na kila mtu  mahali alipo kupanda  miti ili kutekeleza Sera ya Taifa Uhifadhi  wa Mazingira ya Mwaka 2020/21 hatua itakayotupeleka kufikia lengo tulilojiwekea katika Mkakati wa  Utekelezaji wa Sera hiyo,’’alisema Dkt, Kazungu

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Bw.Patience Ntwina alisema kuwa eneo lililopandwa miti lina ukubwa wa hekari mbili ambapo jumla ya miche 600 inayojumisha miche ya  miti ya kivuli na matunda ambayo mahususi katika eneo hilo imepandwa kwa maelekezo ya wataalamu kutoka Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.

‘Tume imeweka mikakati ya kutunza miti hii kwa kuweka miundombinu ya umwagiliaji kwa  muda wa siku tisini(90)ambazo tunaamini  itakuwa imeimarika kwa mizizi kushika udongo,aidha miti hii itakapokuwa itapunguza  joto na kurekebisha hali ya hewa pamoja na kupunguza kazi ya upepo,vimbunga na kukabilianda na mmomonyoko wa udongo’’alisema  Ntwina

Naye, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Mathew P.M.Mwaimu(Jaji Mstaafu) alisema kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja  kati ya haki za binadamu na mazingira naTume  inatambua utekelezaji na upatikanaji wa haki mbalimbali za  binadamu unategemea kwa kiasi kikubwa uwepo wa mazingira yanayowezesha  haki hizo kupatikana