WAAJIRI DODOMA WATAKIWA KULETA TABASAMU KWA WATUMISHI NA WAFANYAKAZI
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kimkoa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Mei 1, 2026 .
Mhe. Senyamule amesema kuwa waajiri wote Serikalini na sekta binafsi wahakikishe kuwa wanafanyakazi kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
Pia Mhe. Senyamule amesisitiza kuwa kauli ya kupeleka tabasamu kwa watumishi inaenda sambamba na kauli ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kupeleka tabasamu kwa wananchi kwa kupeleka huduma bora kwa wananchi.
"Kila anayehusika na haki ya Wafanyakazi basi aitekeleze, ili Watumishi hawa wafurahi, wakitabasamu hawa watawahudima vizuri wananchi na kupeleka tabasamu kwao" amesema Mhe. Senyamule.
Aidha, Mhe Senyamule ametoa wito kwa watumishi kufanya kazi kwakuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utendaji kazi ili kuleta tija kwa mkoa na taifa kwa ujumla.
"Serikali imeendelea kuboresha maslahi ya Watumishi na kuweka mazingira bora, hivyo ni wajibu wenu kufanya kazi kwa bidii" amesema Mhe. Senyamule.
Naye Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bw. Patience Ntwina amesema kuwa watumishi waone umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii ili kujikwakumua kiuchumi.
"Uchumi imara,shindani na endelevu hauwezi kutokea katika mazingira yetu na kufikia Dira ya Taifa 2050 kama hatuta fanya kazi kwa bidii" amesema Bw. Ntwina.
Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yamebebwa na Kauli mbiu isemayo "Wafanyakazi tufanye kazi kwa bidii ili tujenge uchumi imara, shindani na Endelevu"

