ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Wakazi wa Dodoma wanufaika Maadhimisho Miaka 20 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

04 Oct, 2022
Wakazi  wa Dodoma wanufaika Maadhimisho Miaka 20  ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Wakazi wa Jiji la Dodoma  wameendelea  kutembelea mabanda ya maonesho ya kupatiwa elimu pamoja na huduma zinazotolewa na wadau wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala  Bora kuelekea kilele cha maadhimisho ya Miaka  ishirini ya  Tume kinachotarajia kufanyika Septemba 15,2022.

Taasisi mbalimbali zikiwemo za Serikali na Binafsi zinazohusika na masuala ya Haki za Binadamu na Utawala Bora  zimeshiriki maadhimisho hayo kutoka sehemu mbalimbali nchini na kupata nafasi ya kuelezea shuguhli zao kwa Wananchi waliojitokeza kutembelea maonesho hayo.

Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma,Yarerd Jamal alipotembelea maonesho hayo Septemba 13,2022 alisema kuwa amefurahishwa na maandalizi yaliyofanywa na Tume katika maadhimisho hayo na kuwataka wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi kutumia fursa nyingi zinazopatikana katika maadhimisho hayo.

‘’Nimetembelea mabanda mengi katika uwanja huu,nimefurahishwa na jinsi wananchi wanavyopatiwa huduma huduma hapa hasa katika  Wakala ya Usajili ,Ufilisi na Udhamini(RITA) ambapo nimekuta foleni kubwa nawapongeza kwa jinsi mlivyojipanga natoa rai muendelee kuwahamasisha wananchi ambao  bado hawajafika hapa wafanye hivyo,”alisema Mhe. Yarerd

Akiongelea  wadau binafsi waliofika  kuoneshs shughuli zao katika uwanja huo,alisema amejifunza mambo mengi kutoka kwao ambayo awali hakuyajua,na kuwaasa kwamba umefika wakati wa kujitokeza kupitia vyombo mbalimbali vya habari  na kujitangaza ili Watanzania  wawajue  aidha,alitoa rai kwa Taasisi hizo hasa zile  ambazo hazina  Ofisi Dodoma kufanya hivyo.

“Kama mnavyojua  Dodoma ni Makao  Makuu ya Nchi na Serikali nzima  imejikita hapa,ni vizuri Taasisi  binafsi pia mkaweka Ofisi zenu hapa ili muweze kuwahudmia wananchi  kutoka  kila kona ya nchi kwa urahisi,nawakaribisha sana na kama mtakutana na changamoto yoyote katika kutimiza jambo hili karibuni ofisini nipo tayari  ushirikiano,”aliongeza