WANAFUNZI UVINZA WAPATIWA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU.
Utoaji wa elimu ya haki za binadamu na utawala bora katika maeneo ya shule umelenga kujenga uelewa kwa wanafunzi kutambua haki na wajibu wao.
Hayo yameelezwa na Afisa Uchunguzi Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bw. Raphael Mavunde wakati akitoa elimu ya haki za binadamu na utawala bora Mei 07, 2026 katika shule za sekondari za Mazungwe na Ruchugi zilizopo Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
Bw. Mavunde amesema kuwa utoaji wa elimu ya haki za binadamu na utawala bora katika maeneo ya shule ni kwaajili ya kujenga uelewa kwa wanafunzi kuweza kutambua haki na wajibu wao. "Utoaji wa elimu hii itasaidia kujenga jamii inayojua haki za binadamu", amesema Bw. Mavunde.
Pia wanafunzi wameelezwa kuwa utawala bora ni utawala unaozingatia sheria, uwajibikaji na usawa. "Ninyi tunategemea mtakuwa viongozi wa baadae, ni wajibu kutambua kuwa kiongozi bora ni yule anaezingatia haki za binadamu na misingi ya utawala bora" amesema Bw. Mavunde
Naye mwalimu Grace Kinabo amewashukuru maafisa wa THBUB kwa kutoa elimu hiyo ambayo itakua na manufaa kwa sasa na baadae.

