ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Wananchi jitokezeni kupata Msaada wa kisheria Mwenyekiti THBUB

31 Jul, 2023
Wananchi jitokezeni kupata Msaada wa kisheria Mwenyekiti THBUB

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji mstaafu Mathew Mwaimu amewaomba wananchi mkoani Ruvuma kujitokeza ili kutatuliwa changamoto zao kuhusiana na masuala ya kisheria.

Mwaimu ameyasema hayo leo July 22,2023 mkoani Ruvuma katika uzinduzi wa kampeini ya kitaifa ya huduma ya msaada wa kisheria (Mama Samia legal aid campaign).

Amesema kampeini hiyo imeanzishwa na Mhe. Rais kwa lengo la kutoa huduma ya kisheria kwa wananchi wa Tanzania ambapo kampeini hiyo inafanyika katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

“Wananchi waje wapate msaada wa kisheria, kila mmoja mwenye tatizo lake linalo msumbua ambalo amekuwa akishindwa kupata utatuzi akija atashauriwa na kutatuliwa tatizo lake,”amesema.

Aidha ameongeza kuwa kwa changamoto ambayo haitotatulika mara moja itachukuliwa na kupelekwa mbele ya vyombo stahiki kwa madhumuni ya utatuzi.

“Lengo la kampeini kwakweli ni kupata majibu ya haraka, yale maeneo ambayo kidogo yatachelewa kwa kawaida mfano mambo ya polisi, mahakama basi wale wahusika wenyewe katika wiki hizi mbili wataendelea kuwasikiliza wananchi,”ameema