emblem

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu

Muundo wa Tume


Tume inaundwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Makamishna watano (5) na Makamishna Wasaidizi ambao idadi yao haikutajwa kwenye Sheria. Wote huteuliwa na Rais kutokana na mapendekezo ya Kamati ya Uteuzi ambayo inapokea maoni kutoka kwa wananchi.Wajumbe wa Tume ni watu walio na uzoefu na taaluma mbalimbali. Hufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu, na wanaweza kuteuliwa kwa kipindi cha pili kisichozidi miaka mitatu. Chini ya Tume kuna Sekretarieti, ambayo inawajibika kwa kazi za siku hadi siku. Katibu Mtendaji ndiye anayeongoza Sekretarieti na anawajibika kwa Tume kuhusiana na masuala ya kiutawala na utekelezaji wa majukumu ya Tume kama taasisi ya usimamiaji wa haki.

Muundo wa Sekretarieti

Utendaji kazi wa Tume umegawanywa katika Idara, kila moja inaongozwa na Mkurugenzi, na kila Idara imegawanywa katika seksheni chini ya Wakuu wa seksheni. Idara hizo ni zifuatazo:1. Idara ya Malalamiko na Uchunguzi2. Idara ya Elimu kwa Umma, Mawasiliano, Utafitina Nyaraka3. Idara ya Huduma za Kisheria4. Idara ya Utawala na Rasilimali Watu.Aidha, kuna vitengo vifuatavyo katika Tume:

1. Uhasibu na Fedha

2. Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini

3. Ukaguzi wa Ndani

4. Ununuzi na Ugavi

5. Habari na Teknolojia ya Mawasiliano.