27
Wed, Jan
1 New Articles

Top Stories

Grid List

Pongezi kwa Mhe.Job Yustino Ndugai kwa Kuteuliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Press Release

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora(THBUB) inampongeza Mheshimiwa Job Yustino Ndugai (Mbunge wa Kongwa) kwa Kuteuliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Soma Zaidi

 

Pongezi kwa Mhe.Dkt.Tulia Ackson kwa Kuteuliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Press Release

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)inampongeza Mhe.Dkt.Tulia Ackson (Mbunge wa Mbeya Mjini) kwa luteuliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.Soma zaidi

 

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Press Release

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) tumepokea kwa majonzi makubwa taarifa ya kifo cha ghafla cha mpendwa wetu, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa, kilichotokea usiku wa kuamkia leo Julai 24, 2020 huko jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi.Soma zaidi

Hotuba ya Mheshimiwa Bahame Tom Nyanduga, Mwenyekiti wa Tume katika siku ya kupinga mateso na ukatili dhidi ya wazee duniani, tarehe 15 Juni 2017, yaliyofanyika katika ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jengo la Haki, Dar es Salaam. Pakua hotuba kamili

Hotuba ya Mhe. Bahame Tom Nyanduga, Mwenyekiti wa Tume wakati wa hafla ya utoaji tuzo za umahiri wa uandishi wa habari tanzania (EJAT) 2015, ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, aprili 29, 2016. Pakua hotuba kamili

Hotuba ya mwenyekiti wa Tume Mhe. Bahame T. Nyanduga, katika ufunguzi wa mkutano wa wadau kuhusu mikakati ya kukomesha mauaji na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi , tarehe 18 Machi 2015 katika ofisi za Tume. Pakua hotuba kamili

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na  vitendo vya baadhi ya wananchi kuwatumia Watu Wenye Ulemavu kwa kuwafanya ombaomba mitaani kwa lengo la kujiingizia kipato. Aidha, wamekuwa wakiwafanyia vitendo vingine vingi vya udhalilishaji.Soma zaidi

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Jaji mstaafu Mathew Mwaimu (katikati) pamoja na Makamu wake, Mhe. Mohamed Khamis Hamad (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha kujadili taarifa ya Tume ya ukaguzi wa magereza na vituo vya polisi. Wengine kutoka kushoto (waliokaa) ni: Mwakilishi wa Inspekta Jenerali wa Polisi, DCP Fredenand Mtui, Mwakilishi wa Ofisi ya Msajili Mkuu Mahakama ya Rufani, Mhe. Silvia Lushasi na Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Burton Mwasomola. Kikao hicho cha siku moja kimefanyika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma leo Desemba 8, 2020.

News

 

 Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Jaji mstaafu Mathew Mwaimu (katikati) pamoja na Makamu  wake, Mhe. Mohamed Khamis Hamad (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha kujadili taarifa ya Tume ya ukaguzi wa magereza na vituo vya polisi. Wengine kutoka

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji Mstaafu) akitoa tamko la Tume mbele ya vyombo vya habari kuadhimisha Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani ofisini kwake jijini Dodoma leo Desemba 3, 2020

News

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na wadau wote wa haki za Watu Wenye Ulemavu duniani katika kuadhimisha “Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu”  ikiwa na kauli mbiu “Si Kila Ulemavu Unaonekana”.Soma zaidi Soma zaidi

 MAONI YA WANANCHI KUHUSU WAOMBAJI WANAOITWA KWENYE USAILI KWA AJILI YA NAFASI ZA MWENYEKITI, MAKAMU MWENYEKITI NA MAKAMISHNA WA TUME

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ni taasisi huru ya umma na inayojitegemea iliyoanzishwa chini ya Ibara ya 129(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sura ya Pili ya Sheria yenye majukumu ya kuhakikisha kuwa haki za binadamu na utawala zinakuzwa, kulindwa na kuheshimiwa  nchini

Kamati ya Uteuzi  inawaalika  raia wa Tanzania wenye sifa zinazotakiwa kuwasilisha maombi kwa nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna ili  kujaza nafasi zilizo  wazi katika Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.Pakua Habari kamili . Read more

 

TUNAPENDA KUWATANGAZIA WADAU NA WATEJA WOTE WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KWAMBA OFISI ZETU ZILIZOPO JENGO LA TANCOT ZIMEHAMIA JENGO LA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA MTAA WA MKWEPU. HIVYO HUDUMA ZOTE ZITATOLEWA HUKO KUANZIA TAREHE 01 JANUARI, 2019

UTAWALA

Advertisement