ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Mhe. Omar Ali Omar

Omar Ali Omar photo
Mhe. Omar Ali Omar
Makamu Mwenyekiti

Barua pepe: omar.omar@chragg.go.tz

Simu: 0734047775

Wasifu

 

Mhe. Omar Ali Omar (Bhai) ni mtaalamu wa utawala wa umma na usimamizi wa rasilimali watu, mwenye uzoefu mkubwa katika utumishi wa umma, uongozi wa taasisi, utawala, mahusiano ya kikazi na usimamizi wa shughuli za taasisi. Aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) tarehe 28 Oktoba 2026.

Mhe.Bhai amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za juu za kiutendaji na kiutawala katika taasisi za umma nchini. Nyadhifa hizo ni pamoja na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, ambapo alisimamia masuala ya rasilimali watu na utawala; pamoja na Mkuu wa Idara ya Utawala, Mipango na Fedha katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST). Awali, alifanya kazi katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kama Afisa Mwandamizi wa Rasilimali Watu na Afisa Utawala, ambapo pia alihudumu kama Mkufunzi wa Muda. Uzoefu wake wa kazi unajumuisha pia kuhudumu kama Afisa Uhusiano wa Umma na Msaidizi wa Katibu Binafsi wa Mkurugenzi Mkuu katika Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC).

Ana Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe na Shahada ya Sanaa na Sayansi ya Jamii katika Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar. Pia ana Cheti cha Mahusiano ya Kimataifa na Diplomasia kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR), Dar es Salaam pamoja na Cheti cha Ualimu kutoka Chuo cha Ualimu cha Nkrumah.

Katika kipindi cha utumishi wake, Bw. Omar amewahi kuwa na majukumu mbalimbali ya uongozi na usimamizi wa taasisi. Amewahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni katika KIST na Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar. Pia alikuwa mjumbe wa Baraza la Saba la Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na amehudumu katika kamati mbalimbali za taasisi, zikiwemo kamati za ajira, mahafali, rufaa za wanafunzi na uteuzi wa viongozi.

Vilevile, amechangia katika kujenga uwezo wa watumishi kupitia mafunzo aliyoyatoa kuhusu sheria za utumishi wa umma Zanzibar, taratibu za kiutawala katika ofisi za umma, ujuzi wa uongozi, usimamizi wa mabaraza ya taasisi za elimu ya juu, misingi ya maadili na miiko ya utumishi wa umma. Amehudhuria pia mafunzo mbalimbali ya kitaaluma katika maeneo ya utawala na uongozi wa umma, usimamizi wa miradi, usimamizi wa vihatarishi vya kifedha, uandaaji wa bajeti, ukaguzi wa miradi inayofadhiliwa na wafadhili, pamoja na usimamizi na maendeleo ya rasilimali watu. Ni mwanachama wa Chama cha Wataalamu wa Rasilimali Watu na Utawala Tanzania (THRAPA).

Bw. Omar amekuja THBUB akiwa na uzoefu mpana katika utawala wa umma, usimamizi wa rasilimali watu, uongozi wa taasisi na utawala wa sekta ya umma. Uzoefu wake katika kusimamia taasisi za umma, kuratibu shughuli za kiutawala, kushiriki katika michakato ya kufanya maamuzi na kuimarisha maadili ya kitaaluma ni msingi muhimu katika kuchangia utekelezaji wa jukumu la Tume la kukuza na kulinda haki za binadamu pamoja na kuimarisha utawala bora nchini Tanzania.

slot gacor