ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

MWENYEKITI WA THBUB AAPISHWA KUWA MJUMBE WA KAMATI YA USAILI YA WAJUMBE WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI

11 Nov, 2026
MWENYEKITI WA THBUB AAPISHWA KUWA MJUMBE WA KAMATI YA USAILI YA WAJUMBE WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI

 

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Wakili Dunford George Mpelumbe, ameapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Mjumbe wa Kamati ya Usaili ya Wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Uapisho huo umefanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam, Novemba 9, 2026, ukiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria Na. 2 ya Mwaka 2024 inayoweka utaratibu wa kuundwa kwa Kamati hiyo.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 9 (1) cha Sheria hiyo, Kamati ya Usaili imeainishwa kisheria, huku Kifungu cha 9 (2) kikielekeza wajumbe wake kuapa mbele ya Rais kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao.

Kamati hiyo ina wajumbe watano ambao ni Mhe.  George Masaju, Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye ni  Mwenyekiti wa Kamati,  Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla Jaji Mkuu wa Zanzibar, Makamu Mwenyekiti wa kamati, Mhe. Wakili Dunford George Mpelumbe, mjumbe wa kamati, Mhe. Omar Ali Omar, mjumbe wa kamati na Mhe. Balozi Maimuna Kibenga Tarishi, ambapo majukumu yao ni kuchambua maombi, kufanya usaili na kupendekeza majina ya waombaji wanaostahili kwa ajili ya uteuz

slot gacor