ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU  NA UTAWALA  BORA YATOLEWA KWA WANAFUNZI MLEZI.

17 Sep, 2026
ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU  NA UTAWALA  BORA YATOLEWA KWA WANAFUNZI MLEZI.

 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imetoa elimu kuhusu haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlezi iliyopo Jijini Dodoma, Septemba 16, 2026.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo, Afisa wa THBUB, Bw. Innocent Rweyemamu, amesema elimu hiyo imelenga  kuwajengea wanafunzi msingi mzuri wa kuwa raia wanaoheshimu sheria, wanaowajibika, wanaotoa na kupokea taarifa kwa uwazi pamoja na kushiriki katika masuala mbalimbali yanayowahusu.

“Wanafunzi ni viongozi wa kesho, sisi kama THBUB tuna wajibu wa kuwapatia elimu hii,” amesema Bw. Rweyemamu.

Bw.Rweyemamu amesema kuwa  uwazi ni miongoni mwa maingi  wa utawala bora, ambapo wanafunzi wamefundishwa umuhimu wa kusema ukweli, kutoa taarifa sahihi na kutoficha jambo ambalo ni muhimu kwa wengine kulifahamu. 
‘’katika mazingira ya shule, uwazi unaweza kuonekana pale mwanafunzi anapotoa taarifa sahihi kuhusu changamoto inayomkabili, pamoja na viongozi wa wanafunzi na walimu kutoa taarifa kwa uwazi kuhusu mambo yanayowahusu wanafunzi’’amesema Bwa.Rweyemamu.

Kwa upande wake, Afisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. David Piniel alitoa elimu kuhusu haki muhimu za binadamu na kueleza kuwa haki ya kuishi ni miongoni mwa haki za binadamu inahusisha kupata mazingira salama yanayomwezesha kuishi na kukua, huku haki ya kulindwa ikihusisha ulinzi dhidi ya ukatili, unyanyasaji na vitendo vinavyoweza kumdhuru mtoto. Aidha, ameeleza kuwa haki ya kupata elimu ni muhimu katika kumwezesha mtoto kupata maarifa na ujuzi wa kujenga maisha yake na kutimiza ndoto zake.

slot gacor