ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

WANAFUNZI WATAKIWA KUSOMA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI KUJUA HAKI ZAO

17 Sep, 2026
WANAFUNZI WATAKIWA KUSOMA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI KUJUA HAKI ZAO

 

Wanafunzi wametakiwa kujenga utamaduni wa kusoma na kuelewa Katiba pamoja na sheria za nchi ili waweze kuzifahamu haki zao za msingi na kutekeleza wajibu wao kama raia wenye nafasi muhimu katika maendeleo ya Taifa.

Rai hiyo imetolewa na Afisa Uchunguzi Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bw. Moses Mfundo, alipokuwa akitoa elimu ya haki za binadamu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Viwandani iliyopo  Jijini Dodoma.

Bw. Mfundo Amesema uelewa wa Katiba na sheria ni muhimu kwa mwanafunzi kwani humwezesha kutambua haki alizonazo, mipaka ya haki hizo pamoja na wajibu unaoambatana nazo.

Aidha amesisitiza kuwa elimu ya haki za binadamu inapaswa kupewa kipaumbele mashuleni kwa kuwa wanafunzi ni sehemu muhimu ya jamii na viongozi wa kizazi kijacho.  kuwajengea uelewa wa haki za binadamu wakiwa katika umri wa shule, wanafunzi huandaliwa kuwa raia wanaoheshimu haki za wengine, wanaotambua wajibu wao na wanaoshiriki katika masuala ya kijamii kwa kuzingatia misingi ya sheria na utawala bora.

Ameongeza kuwa elimu hiyo pia inalenga kuwajengea wanafunzi uwezo wa kutambua na kukataa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwemo ukatili, ubaguzi, unyanyasaji na vitendo vingine vinavyokiuka utu wa binadamu na kutumia njia halali na salama katika kutoa taarifa au kutafuta msaada pale wanapobaini ukiukwaji wa haki.


Kwa upande wao, wanafunzi hao wameeleza kufurahishwa na mafunzo hayo wakisema yamewasaidia kupata uelewa mpana kuhusu haki zao za msingi, wajibu wao na namna ya kuzilinda. Wamesema wataendelea kusoma na kujifunza Katiba na sheria za nchi ili kuongeza uelewa wao na kuwa mabalozi wa haki za binadamu katika shule na jamii kwa ujumla.

Elimu ya haki za binadamu mashuleni ni sehemu muhimu ya kuwaandaa vijana kuwa mabalozi wa haki za binadamu na utawala bora katika familia, shuleni na katika jamii kwa ujumla. Kupitia elimu onayotolewa na THBUB, wanafunzi hujifunza kuheshimu utu wa kila mtu, kuthamini usawa, kutatua migogoro kwa njia za amani na kushiriki kikamilifu katika kujenga jamii inayozingatia haki, wajibu na utawala wa sheria.

slot gacor