ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

HAKI ZA BINADAMU NI NGUZO MUHIMU KATIKA KUSIMAMIA UTAWALA BORA.

16 Sep, 2026
HAKI ZA BINADAMU NI NGUZO MUHIMU KATIKA KUSIMAMIA UTAWALA BORA.

Katika kuhakikisha haki za Watoto zinalindwa na kuhifadhiwa, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imetoa elimu ya  Haki za binadamu na Utawala Bora katika Shule ya Msingi Makulu iliyopo Jijini Dodoma, Septemba 15,2026.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo Afisa wa Tume   ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi.Florence Chaki amesema kuwa haki za binadamu ni haki za msingi ambazo binadamu anatakiwa kuzipata pindi anapozaliwa.

Bi.Chaki amesema kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imetaja haki mbalimbali  ikiwemo haki ya kuishi,uhuru wa kutoa maon,haki ya kumilki mali na nyingine, haki hizo zote kila binadamu anatakiwa kuzipata bila ubaguzi wowote.


Aidha, Bi.Chaki amewaeleza wanafunzi hao kuwa wanayo haki ya kupata elimu na kulindwa dhidi ya masuala ambayo yataweza kuwafanya kuvunjiwa haki zao,pia amewasisitiza kuhusu wajibu wao wanapokuwa shuleni na katika jamii,ikiwemo kuepuka kukaa katika mazingira hatarishi yatakayoweza kupelekea haki zao kuvunjwa

‘’watoto mnayo haki ya kulindwa ,ni wajibu wenu pia kujiepusha kukaa katika mazingira yatakayo wavunjia haki zenu,mtoe taarifa mnapopata changamoto”amesema Bi.Chaki 

Pia Bi.Florence amepafursa kuwaelezea wanafunzi hao kuhusu THBUB na Majukumu yake,ambapo amewaleza wanafunzi hao kuwa THBUB inajukumu la kulinda na kuhifadhi  haki za binadamu na wajibu kwa jamii kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi,kupokea malalamiko ya uvunjaji wa haki za binadamu,kufanya utafiti,kutoa na kueneza elimu kwa umma kuhusu haki za binadamu na utawala bora

‘’Majukumu haya yameundwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977" amesema Bi.Chaki

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bwa.Amoni Sebyiga ametoa shukrani kwa THBUB kwakufika shuleni hapo na kutoa elimu ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na kuwakumbusha wanafunzi  hao wajibu wao.

slot gacor