ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB KUSHIRIKIANA NA WADAU KATIKA KULINDA HAKI ZA BINADAMU

14 Sep, 2026
THBUB KUSHIRIKIANA NA WADAU KATIKA KULINDA HAKI ZA BINADAMU

 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imejipanga  kushirikiana na wadau mbalimbali katika kulinda haki za binadamu na utawala bora nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji Bi. Suzan Ndeona wakati wa kikao baina ya THBUB na   ujumbe wa ubalozi wa Norway Tanzania katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Jengo la hifadhi ya Mfuko wa Jamii kwa Watumishi wa Umma,Makole Jijini Dodoma Septemba 10,2026.

Bi Ndeano amesema katika kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa inaendelea kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi katika kutoa elimu kwa jamii. 
“ Tunashirikiana na  asasi za Kiraia na mashirika ya Kimataifa ili kuona jamii inatambua umuhimu wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora” Amesisitiza.

Aidha, aliongeza kuwa mara nyingi THBUB imekuwa ikifanya mijadala kuhusu masuala ya haki za binadamu na biashara na masuala ya ukatili wa kijinsia, wakati wa mchakato wa kufanya tathmini ya hali ya haki za binadamu nchini pamoja na kushirikiana katika miradi mbalimbali ikiwemo masuala ya Bahari endelevu kwa kuangalia haki za wavuvi wadogo.

Sambamba na hayo  , Bi.Ndeona amesema kuwa THBUB imetoa elimu kwa makundi mbalimbali  wakiwemo Watendaji wa Kata na Vijiji, Madiwani, Waandishi wa habari, wawakilishi wa vyama vya siasa,  na Askari wa Jeshi la polisi. 
‘hatua yakutoa elimu ni kuendelea kuimarisha utawala bora unaombatana na haki za binadamu”amesema bi.Ndeona

Licha ya utoaji elimu Bi.Ndeona amesema kuwa THBUB inajukumu la kufanya utafiti na kufanya uchunguzi juu ya masuala ya uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora

Naye, Mtaalamu wa Masula ya Siasa kutoka ubalozi wa Norway Bwa. Oyvindi Gressetvold  amesema  kupitia kikao hicho ameweza kuelewa kuhusu THBUB na majukumu ya THBUB na  kwa pamoja watakaa na   kuona maeneo watakayoweza shirikiana na THBUB.

slot gacor