ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

MWENYEKITI  THBUB AFUNGUA RASMI JUKWAA LA 11 LA UZIDUAJI 2026

13 Nov, 2026
MWENYEKITI  THBUB AFUNGUA RASMI JUKWAA LA 11 LA UZIDUAJI 2026

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Wakili Dunford George Mpelumbe, amefungua Jukwaa la 11 la Uziduaji 2026, lilnalofanyika  katika  ukumbi  wa Mabeyo jijini Dodoma, Desemba 12, 2026.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo,  Mhe. Mpelumbe amesema THBUB inatambua umuhimu wa sekta ya uziduaji na uhusiano wake wa moja kwa moja na haki za binadamu, hususan kwa jamii zinazoathiriwa na shughuli za uchimbaji wa madini,  mafuta na gesi.

Amesema  THBUB, kwa mujibu wa mamlaka yake ya kikatiba,  ina wajibu wa kusimamia na kuhakikisha uhifadhi na utekelezaji wa misingi ya haki za binadamu na utawala bora katika taasisi za Serikali na sekta binafsi, ikiwemo sekta ya uziduaji unazingatiwa.

Katika kutekeleza wajibu huo,  Tume inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha  kanuni   na miongozo ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu na Biashara (UNGPs) zinaingizwa katika mifumo ya kitaasisi,  kisheria na kisera nchini,  ili kuimarisha uwajibikaji wa biashara na kulinda haki za binadamu katika shughuli za uwekezaji.

"Sisi kama Tume  tumechukua  hatua muhimu katika kuhakikisha kwamba sekta ya uziduaji inazingatia misingi ya haki za binadamu na utawala bora," amesema  Mhe.  Mpelumbe.

Aidha, amewahimiza washiriki wa jukwaa  hilo kushiriki kikamilifu kwa kutoa maoni, uzoefu na mapendekezo yatakayosaidia Serikali na THBUB kuimarisha uwajibikaji na kuhakikisha wadau wote katika sekta hiyo wanazingatia misingi ya  haki za binadamu na utawala bora pamoja na matakwa ya haki za binadamu.

Jukwaa la 11 la Uziduaji 2026 linaongozwa na kaulimbiu isemayo: "Kutoka Utajiri wa Rasilimali Asilia Hadi Ustawi wa Pamoja: Je, Tanzania Ipo Tayari kwa Enzi Mpya ya Uziduaji?"

Kaulimbiu hiyo inasisitiza umuhimu wa kuhakikisha uwekezaji katika sekta ya uziduaji unaleta manufaa mapana kwa Taifa kwa kuongeza thamani ya rasilimali asilia nchini, kukuza viwanda, kuendeleza ujuzi na teknolojia, kuongeza ajira zenye staha pamoja na kupanua ushiriki wa wazawa katika mnyororo wa thamani.

Kupitia Jukwaa hilo, wadau wanapata fursa ya kujadili namna bora ya kuhakikisha utajiri wa rasilimali asilia unatafsiriwa kuwa maendeleo jumuishi na ustawi wa wananchi, huku haki za binadamu, uwajibikaji na utawala bora vikiendelea kuwa msingi wa shughuli zote za uwekezaji katika sekta ya uziduaji.

slot gacor