ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAITAMBULISHA OFISI YA TAWI JIPYA MBEYA

12 Nov, 2026
THBUB YAITAMBULISHA OFISI YA TAWI JIPYA MBEYA

 Afisa Mfawidhi wa tawi la Mbeya la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Bi. Ritha Malisa amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Balandya Mayuganya Elikana, kwa lengo la kuitambulisha rasmi  ofisi ya tawi hilo iliyofunguliwa Novemba 10, 2026.

Akizungumza wakati wa kikao hicho,   Bi. Malisa amesema kuanzishwa kwa ofisi hiyo ni sehemu ya jitihada za THBUB za kusogeza huduma karibu na wananchi zinazohusiana na ulinzi na uhifadhi wa haki za binadamu  na misingi ya utawala bora.

Ameeleza kuwa kupitia ofisi hiyo, Tume inalenga kupanua wigo wa utoaji wa huduma kwa wananchi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, sambamba na kuimarisha ushirikiano na taasisi za Serikali  na binafsi pamoja na wadau. 

"Kuanzishwa kwa ofisi hii kutarahisisha upatikanaji wa huduma zinazotolewa na Tume kuhusu haki za binadamu na uzingatiwaji wa misingi ya utawala bora," amesema Bi. Malisa

slot gacor