ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAWAHAKIKISHIA WANANCHI UTATUZI WA HARAKA WA MALALAMIKO KUHUSU HAKI ZA BINADAMU.

13 Nov, 2026
THBUB YAWAHAKIKISHIA WANANCHI UTATUZI WA HARAKA WA MALALAMIKO KUHUSU HAKI ZA BINADAMU.

 

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Wakili Dunford George Mpelumbe, amewahakikishia wanachi wa Zanzibar kuwa Tume hiyo imejipanga vyema katika kupokea, kuchunguza na kutatua kwa wakati na usawa, malalamiko yote ya uvinjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora yanayowasilishwa katika ofisi za Tume hiyo zilizopo Zanzibar.

Mhe. Mpelumbe ameyasema hayo jana Novemba 11, 2026, alipozungumza na waandishi wa habari wa vyombo katika Ofisi za Tume zilizopo eneo la Mombasa, Mkoa wa Mjini Magharibi.
 
Akitaja majukumu ya Tume hiyo kwa waandishi hao, Mwenyekiti Mpelumbe amewaeleza waandishi hao kwamba mbali ya majukumu mengi THBUB iliyonayo, inatoa Elimu kwa Umma, kusimamia mikataba ya kimataifa kwa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mikataba yote ya kikanda na kimataifa inayohusu haki za binadamu ambayo Tanzania imeridhia.

Pia, ameeleza namna ya Tume inavyoendelea na kushughulikia malalamiko ya wananchi yanayowasilishwa  katika ofisi za Tume zilizopo maeneo mbalimbali ya nchini zikiwemo Ofisi ya Makao Makuu Dodoma, Ofisi ya Zanzibar na ofisi za matawi zilizopo Pemba, Mwanza, Dar es Salaam, Tabora, Mtwara na Mbeya.

Aidha, Mhe. Mpelumbe ameendelea kutoa wito kwa jamii na wadau wa haki za binadamu kuendeleza ushirikiano wa pamoja uliopo baina yao na Tume, sambamba na kuendeleza kujenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu na misingi ya utawala bora nchini.

Naye Makamu Mwenyekiti, Mhe. Omar Ali Omar Bhai, wakati akijibu swali la waandishi kuhusu mkakati mpya wa Tume wa kutosubiri malalamiko ofisini pekee, amefafanua mwelekeo wa utendaji kazi za Tume wa kuchukua hatua kwa haraka na wakati kama ulivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Tume hatutakuwa watu wa kukaa maofisini na kusubiri wananchi waje, badala yake tumejipanga kikamilifu kuchukua hatua za haraka na za makusudi kutambua, kuchunguza, na kushughulikia changamoto zote za haki za binadamu na utawala bora mara zinapojitokeza katika jamii," amesisitiza Mhe. Omar.
 
Aidha, Makamu Omar ametoa wito kwa wananchi na jamii kwa ujumla vikiwemo vyombo vya habari, kuacha woga na kuwa huru kuifikia Tume kwani ndio chombo chao kikuu cha utetezi wa misingi ya haki na utu. 

Huu ni mkutano wa kwanza na vyombo vya habari kwa Zanzibar, tangu uongozi mpya ulipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuapishwa hivi karibuni.

slot gacor