ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

WATUMISHI THBUB WATAKIWA  KUENDANA NA KASI YA KIDITALI

12 Nov, 2026
WATUMISHI THBUB WATAKIWA  KUENDANA NA KASI YA KIDITALI

 

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Wakili Dunford George Mpelumbe amewataka watumishi wa Tume  Ofisi ya Zanzibar kubadili mfumo wa utendaji kazi wao ili kuendana na kasi ya teknolojia ya kisasa ya kidijitali katika kutekeleza majukumu ya THBUB. 

Mhe. Mpelumbe ameyasema hayo katika  Ofisi za THBUB zilizopo eneno la Mombasa Mtaa wa tawini Mkoa wa Mjini Magharibi  Novemba 10, 2026 alipozungumza na watumishi wa ofisi hiyo. 

Amesema, matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika kupokea, kuchakata na kufuatilia malalamiko ya ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora yanarahisisha utendaji kazi.

Mhe. Wakili Mpelumbe amebainisha kuwa mabadiliko ya kidijitali na mapinduzi ya teknolojia yanarahisisha uwazi, kudhibiti muda  na kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa wakati katika kushughulikia na kufanyia kazi malalamiko yao.

Aidha, amesisitiza suala la ushirikiano kwa watumishi hao ambapo amesema  ufanisi wa Tume hutegemea zaidi upendo, ushirikiano na kujituma miongoni mwa wafanyakazi. 

“Mazingira bora ya kazi yanajengwa pale watumishi wanaposaidiana na kuheshimiana."Hatuwezi kuwahudumia wananchi vizuri ikiwa sisi wenyewe hatupendani au hatushirikiani, Upendo na mshikamano ndio nguzo kuu itakayotufanya tuwe timu moja madhubuti," amesisitiza Mhe. Wakili Mpelumbe

Naye Makamu Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Omar Ali Omar Bhai amewataka  watumishi hao kuendelea kufanyakazi zao kwa usiri wa hali ya juu ili kuendelea kujenga imani kwa jamii wanayoitumikia.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mtendaji Bw. Juma Msafiri Karibona amewapongeza viongozi hao kwa kuaminiwa na kuteuliwa  na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Mungano, wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutumikia nafasi zao.

slot gacor