ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

MWENYEKITI WA THBUB AKUTANA NA KATIBU MKUU KIONGOZI ZANZIBAR

18 Nov, 2026
MWENYEKITI WA THBUB AKUTANA NA KATIBU MKUU KIONGOZI ZANZIBAR

 

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Wakili Dunford George Mpelumbe, amesema Tume hiyo itaendeleza ushirikiano wake wa karibu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji wa majukumu yake ya Kikatiba ikiwemo kutoa elimu kwa umma na kushughulikia malalamiko ya wananchi kwa haki na bila upendeleo.
 
Mhe. Dunford akiwa na ujumbe alioongozana nao, ameyasema hayo Ikulu, Zanzibar walipokutana na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Mansura Mosi Kassim kwa lengo la kujitambulisha mara baada ya kuteuliwa na kuapishwa kwake na Rais wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, hivi karibuni.

Aidha, Wakili Dunford amemshkuru Katibu Mkuu Kiongozi Mansura kwa mapokezi mazuri na kupongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha Utawala Bora na upatikanaji wa haki kwa wananchi. 

Kwa upande wake, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ, Bi. Mansura Mosi Kassim, amewapongeza Mhe. Wakili Mpelumbe na uongozi mpya wa THBUB kwa kuaminiwa kwao na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushika nyadhifa walizonazo.
 
Katika hatua nyengine, Katibu Mkuu Kiongozi Mansura ameuahidi uongozi huo wa THBUB kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa Tume hiyo ili kuhakikisha malengo ya kulinda haki za binadamu na kuimarisha uwajibikaji katika utumishi wa umma na misingi ya utawala bora yanafikiwa kwa ufanisi.
 
Ziara hiyo ya kikazi ya Mwenyekiti wa THBUB ameongozana na Makamu wake Mhe. Omar Ali Omar na Naibu Katibu Mtendaji, Bw. Juma Msafiri Karibora imelenga kujitambulisha rasmi kwa uongozi wa juu wa THBUB kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kujadili mikakati ya kuimarisha ushirikiano baina ya THBUB na taasisi za SMZ katika kukuza, kulinda na kutetea haki za binadamu na misingi ya utawala bora visiwani Zanzibar.

Mkutano huo ni mwendelezo wa ziara za kujitambulisha za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wake tangu walipoapishwa mapema mwezi huu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kukabidhiwa ofisi rasmi. 

Pia, Mhe. Mpelumbe akiongozana na Makamu Mwenyekiti wake, Mhe. Omar Ali Omar na Naibu Katibu Mtendaji, Bw. Juma Msafiri Karibona walikutana na Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar CP Kombo Khamis Kombo kwa mazungumzo ya kikazi.

 

slot gacor