ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB: WANANCHI WAFUATE TARATIBU WANAPODAI HAKI ZAO.

12 Jul, 2026
THBUB: WANANCHI WAFUATE TARATIBU WANAPODAI HAKI ZAO.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bw. Patience Ntwina, amewataka wananchi kufuata taratibu za kisheria na kuheshimu mamlaka zilizopo wanapodai haki zao ili kuendelea kudumisha amani, utulivu na utawala bora nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika banda la THBUB kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Bw. Ntwina amesema mafanikio ya tume hiyo yanaonekana wazi kupitia kuimarika kwa mazingira ya wananchi kufurahia haki na uhuru wao bila hofu.

Amesema kwa sasa wananchi wanaweza kutembea kwa uhuru na kukaa katika mabanda ya mpira wakifuatilia mechi za Kombe la Dunia linaloendelea bila wasiwasi wowote, hali ambayo inaashiria kuimarika kwa usalama na uhuru wa wananchi.

“Ni muhimu wananchi wakaendelea kufuata taratibu zilizowekwa na kuheshimu mamlaka zilizopo wanapodai haki zao. Hii ndiyo njia bora ya kuendelea kulinda amani na kuhakikisha haki za kila mmoja zinazingatiwa,” amesema Bw. Ntwina.

Ameongeza kuwa hali hiyo inaonyesha wazi kuwa THBUB kwa kushirikiana na Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na utulivu, amani na mazingira yanayowezesha haki za binadamu kulindwa na kuheshimiwa.

Bw. Ntwina amesema THBUB itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kuhamasisha na kulinda haki za binadamu pamoja na kusimamia misingi ya utawala bora kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla.

slot gacor