THBUB YASHIRIKI UZINDUZI WA NYARAKA NA MIFUMO YA KITAASISI.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeshiriki katika hafla ya uzinduzi wa nyaraka na mifumo ya kitaasisi iliyoandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, iliyofanyika Novemba 26, 2026, katika Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha.
Ushiriki wa THBUB katika hafla hiyo uliwakilishwa na Mwenyekiti Mhe.Wakili Dunford George Mpelumbe, Makamu Mwenyekiti Mhe. Omar Ali Omar Bhai pamoja na baadhi ya viongozi wa Menejimenti ya Tume, ikiwa ni sehemu ya kujifunza mbinu bora za uandaaji na usimamizi wa nyaraka na mifumo ya kitaasisi.
"tumeshiriki hafla hii kwa lengo la kujifunza na kupata uzoefu katika uandaaji wa nyaraka na mifumo ya kitaasisi inayosaidia kurahisisha utendaji kazi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi". Amesema Mhe. Wakili Mpelumbe
Miongoni mwa nyaraka na mifumo iliyozinduliwa ni Mpango Mkakati, Sera ya Mawasiliano, Mkataba wa Huduma kwa Mteja, Mpango wa Maendeleo ya Rasilimali Watu, pamoja na mfumo wa maktaba mtandao.
Nyaraka na mifumo hiyo inalenga kuimarisha utendaji wa taasisi, kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma, kurahisisha upatikanaji wa taarifa pamoja na kuboresha uwajibikaji kwa wananchi.

