THBUB YATEMBELEA OFISI ZA POLISI MBEYA
Mfawidhi waTawi la Mbeya la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ( THBUB), Bi. Ritha Malisa ametembelea Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, iliyopo Mbeya Mjini na kufanya mazungumzo na Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ACP Wilbert Mica Siwa Nivemba 20, 2026.
Bi. Ritha Malisa, amesema kuwa ziara hiyo inalenga kujitambulisha na kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji baina ya taasisi hizo katika masuala ya haki za binadamu na utawala bora.
Aidha, Bi. Malisa amesema kuwa katika ziara hiyo, THBUB imepata fursa ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu haki za binadamu na utawala bora, pamoja na kupata ufafanuzi kuhusu malalamiko yaliyowasilishwa na wananchi, hatua inayolenga kuimarisha mawasiliano na ushirikiano katika kushughulikia masuala hayo.
Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za THBUB za kujenga na kuimarisha ushirikiano na taasisi za umma katika kukuza, kulinda na kutetea haki za binadamu, pamoja na kuhimiza uzingatiaji wa misingi ya utawala bora.

