ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

WATUMISHI THBUB ZANZIBAR WAHIMIZWA UBUNIFU NA WELEDI KAZINI

23 Nov, 2026
WATUMISHI THBUB ZANZIBAR WAHIMIZWA UBUNIFU NA WELEDI KAZINI

 

Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Ofisi ya Zanzibar, wamehimizwa kuzingatia ubunifu, weledi na kutenda haki bila upendeleo katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuongeza ufanisi na kuboresha huduma kwa wananchi.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Wakili Dunford George Mpelumbe wakati wa kikao kazi cha kutathmini  utendaji kazi na kuweka mikakati ya kuboresha utendaji kazi  kilichofanyika Mombasa, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar leo, Novemba 20, 2026 . 

Mhe. Wakili Mpelumbe amesisitiza umuhimu wa watumishi kuzingatia misingi ya haki, usawa na maadili ya utumishi wa umma, akieleza kuwa misingi hiyo ni muhimu katika kujenga imani ya wananchi kwa Tume, hususan katika kushughulikia malalamiko ya ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Aidha, amewataka watumishi kutumia fursa za maendeleo ya teknolojia kubuni njia bora na za kisasa za mawasiliano zitakazowezesha Tume kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa wakati na kurahisisha upatikanaji wa huduma.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mtendaji, Bw. Juma Msafiri Karibona, amemhakikishia Mwenyekiti kuwa maelekezo na ushauri uliotolewa vitafanyiwa kazi ili kuongeza ufanisi na kuhakikisha malengo ya Tume yanafikiwa.

Vilevile, amewahimiza watumishi kuendelea kuwa wasikivu na wenye kujali mahitaji ya wananchi wanapotekeleza majukumu yao, akibainisha kuwa ziara ya uongozi wa juu wa Tume Zanzibar imeongeza matumaini ya kupatiwa ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili Ofisi ya Unguja na Tawi la Pemba.

Ameeleza kuwa hatua hiyo inatarajiwa kuimarisha mazingira ya utendaji kazi, kuongeza ari ya watumishi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi wa Zanzibar.

slot gacor