ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAZINOA TAASISI ZA SMZ PEMBA KUHUSU HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

16 Oct, 2026
THBUB YAZINOA TAASISI ZA SMZ PEMBA KUHUSU HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ofisi ya Zanzibar, imetoa  elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa watumishi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza katika mafunzo hayo,  yaliyofanyika  Gombani, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba, Naibu Katibu Mtendaji THBUB, Bw. Juma Msafir Karibona, aliwaeleza watumishi hao juu ya umuhimu wakutambua Haki za Binaadamu na misingi ya Utawala Bora.

Amesema, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa mpana watumishi hao ili wawe mabalozi wazuri wa kueneza dhana nzima ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa jamii zao.

Aidha, Bw. Karibona alizisitiza suala la ushirikiano baina ya Tume, taasisi za SMZ na wadau wengine wa haki za binadamu ili kuendelea kulinda na kukuza haki za binadamu na misingi ya Utawala Bora nchini.

Naye, Afisa Mdhamini Ofisi ya Rais Ikulu, Kisiwani Pemba Bi. Shuweikha Abdalla Omar ameishukuru THBUB kwa kuandaa mafunzo hayo na kuisihi Tume hiyo kuendeleza juhudi za kutoa elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora katika ngazi zote ili jamii nzima itambue haki na wajibu wao Kisheria.

Kwa upande wake, Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Bw. Ali Salim Matta Alisifu fursa ya mafunzo hayo na kueleza kwamba yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha utendaji wenye uwazi, uwajibikaji, na ushirikiano miongoni mwa watumishi wa umma visiwani humo.

Ufunguzi wa mafunzo hayo pia ulihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe. Rashid Hadid Rashid, ambaye alionyesha utayari wa mkoa huo katika kuunga mkono juhudi za THBUB katika kusimamia haki za binadamu na kuimarisha misingi ya utawala bora kuanzia ngazi za Shehiya, Wilaya hadi Mikoa

slot gacor