ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

WANAFUNZI WAASWA KUTOFUMBIA MACHO VITENDO VYA UKATILI

17 Sep, 2026
WANAFUNZI WAASWA KUTOFUMBIA MACHO VITENDO VYA UKATILI


Wanafunzi wameaaswa kutokaa kimya wanapofanyiwa vitendo vya ukatili au kushuhudia uvunjwaji wa haki za binadamu, bali watoe taarifa kwa mtu wanayemwamini au uongozi wa shule. 

Hayo yamesemwa na Afisa Uchunguzi Mkuu Msaidizi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THUBU) Bw. Halfan Botea wakati akitoa elimu na kuanzisha Klabu ya Haki za Binadamu katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo iliyopo jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo, Bw. Botea amesema kuwa ni muhimu watoto kujua kuwa wanayo haki ya kulindwa dhidi ya vitendo vya ukatili na wanapaswa kusema pale haki zao zinapokiukwa.

“Tunataka wanafunzi mfahamu haki zenu na mjue ni wapi mahali sahihi pa kwenda kutoa taarifa mnapofanyiwa ukatili au mnapoona haki za binadamu zinavunjwa. Msikae kimya; toeni taarifa kwa mtu mnayemwamini au uongozi wa shule ili muweze kupata msaada unaostahili.” amesema Bw. Botea.

Kwa upande wake Askari wa Jeshi la Polisi Meja Kamani Shigela ameeleza kuwa sheria za nchi zinawahusu watu wote, wakiwemo wazazi, hivyo hawapaswi kusita kutoa taarifa endapo watafanyiwa vitendo vya ukatili na wazazi wao au mtu mwingine yeyote.

Meja Kamani amewataka wanafunzi kutumia njia sahihi za utoaji wa taarifa ili mamlaka husika ziweze kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria. 

THBUB imeendelea kutoa elimu na kufungua Klabu za Haki za Binadamu mashuleni ili kuwajengea wanafunzi uelewa wa haki za binadamu na wajibu wao katika jamii.

slot gacor