ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

WANAWAKE WAVUVI MTWARA WAELIMISHWA KUTOA TAARIFA JUU YA UVUNJIFU WA HAKI ZAO

18 Jun, 2026
WANAWAKE WAVUVI MTWARA WAELIMISHWA KUTOA TAARIFA JUU YA UVUNJIFU WA HAKI ZAO

Wanawake wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi na biashara ya samaki katika Manispaa ya Mtwara-Mikindani wamehimizwa kutoa taarifa juu ya vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu ili viweze kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Wito huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bw. Patience Ntwina wakati wa mafunzo ya haki za binadamu yaliyotolewa kwa wanawake wanaofanya shughuli za uvuvi mdogo katika eneo la Feri, Kata ya Shangani.

Bw. Ntwina amesema ni muhimu kwa wanawake hao kutambua haki zao na kutumia mifumo ya kisheria kutoa taarifa za vitendo vinavyokiuka haki hizo ili kuimarisha ulinzi wa haki zao na ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi.

Aidha, amesema THBUB itaendelea kutoa elimu ya haki za binadamu na kupokea malalamiko ya wananchi kwa lengo la kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu na utawala bora nchini.

Kwa upande wao, wanawake walioshiriki mafunzo hayo wameishukuru THBUB kwa kuwapatia elimu na fursa ya kueleza changamoto zinazowakabili ikiwemo uwepo wa madalali wanaoathiri biashara ya samaki, ukosefu wa ulinzi wa mali zao na kubebeshwa majukumu makubwa ya kifamilia.

Wamesema changamoto hizo zinaathiri kipato na ustawi wa familia zao, hivyo wameiomba THBUB na mamlaka husika kuchukua hatua za kulinda haki zao na kuweka mazingira salama na yenye usawa katika shughuli za uvuvi na biashara ya mazao ya baharini.

Mafunzo hayo yameelezwa kuwa hatua muhimu ya kuongeza uelewa wa haki za binadamu na kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

slot gacor